Maadhimisho Ya Mashujaa Wetu

Printer-friendly versionPDF version

Leo ilikuwa siku kubwa. Siku ambayo sote tuliwakumbuka na kuwasheherekea baadhi ya Wakenya wazalendo ambao walituunda sisi, walitupangia nchi tukawa tulivyo leo, walihatarisha maisha yao kutufanya sisi tuwe kama tulivyo leo; walijitolea mhanga kuhakikisha kwamba wewe na mimi na  mimi na wewe, tumepata vifaa muhimu  vya kukabiliana na maisha  kama vile elimu ambayo ilikuwa haba katika siku za wakoloni. Ingawa hafla hio ilifanyika leo nchini Kenya na sehemu zinginezo ulimwenguni, majina ya mashujaa hao hayakusikika kamwe katika hotuba zote tulizozizikia.

Leo nalitafakari hili la Wahenga, kwamba " Kwa mwoga huenda kicheko, kwa shujaa huenda kilio." Ni kwa sababu shujaa ni mtu mwenye moyo thabiti,anayeweza kukabili mambo, hata kama ni ya hatari, bila ya khofu. Shujaa ni mtu jasiri. Shujaa huiacha mke, watoto na jamii yake ili  kuwawakilisha na kuwapigania wananchi wazinyakue haki na masuala mengine ambayo yanawakabiri. Shujaa hayatendi haya akiwa na tamaa yoyote. Anafanya hivyo kwa kujitolea. Shujaa hatendi haya akiwa na kusudio la kujinufausha kwa njia yoyote. Yuafanya haya bure bilashi, bila kutarajia malipo yoyote au mshahara wowote. Katika siku nizikumbakazo mimi, shujaa na mwanaharakati kama Dedan Kimathi anafuzu kusheherekewa. Ni kwa sababu hata baada ya kuwakomboa Wakenya kutoka kwa Wabeberu walio tukandamiza kwa miongo na dahara, shujaa huyu alifariki akiwa maskini huku waliopigania uhuru naye wakipora na kumiliki maelfu na maelfu na ekari za mashamba, nyumba na mifugo, huku wakiwapea wazungu masaa 48 kurudi kwao Uingereza.Kwa maoni yangu, wanaharakati kama Kenyatta, Kubai, Moi, na wengineo waliosukumwa gerezani huko Kapenguria hawaangukii katika orodha hii ya mashujaa tunaowasheherea leo.

Kumechipuka mashujaa mamboleo nchini mwetu ambao kwa kweli watishia kuwepo kwa ushujaa kati ya watoto wetu hapo siku sijazo. Katika pitapita zangu za kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, kumetokea sampuli ya baadhi ya Wakenya ambao ushujaa kwao si kuwafikiria wengine ila ni kujifiria wao binafsi hasa wanapowahudumia wananchi. Tunawapa dhamana ya kuwa wapangaji wa miji yetu, wasimamizi wa sera za sheria zetu, wasimamizi wa pesa zetu zisivunjwe, tukawapa madaraka wayatakayo, lakini wao wakalala usingizi, usingizi wa pono. Ramani za miji wakazifungia kabatini ziliwe na panya. Diposa kukachipuka mitaa kama ile ya Kibera, Mukuru, Kia Maina na kadharika, ambako wananchi, kwa sababu hawana elimu, wala uwezo wa kuridhisha, kifedha, wakaanza kujenga makazi wasitiri familia zao. Mwishowe, wanakosa matumaini. Miaka karibu hamsini tangu uhuru, wanangoja tu, mara moto unatokea na kuyachoma mabanda yao yote. Viongozi wanaowawakilisha bungeni, wanatazama na kupayuka tu, mara wanasahaulika.

Laiti kama wawakilishi wa wananchi, haswaa wabunge wajulikanao kama MPIgs, wangeutimiza wajibu wake itakikanavyo, leo hatungekuwa na ujenzi holela. Leo tungeliwakumbuka Rais Kibaki, Waziri Mkuu Raila, Mawaziri, MPIgs, wakuu wa wilaya, na watumishi wengene serikalini, kwa kuboresha maisha ya Wakenya wote kwa kuanzisha miundombinu inayoweza kuwakwamua kutoka majanga tuyaonayo leo. Tungeliwashangilia na kuwasujudia kwa kuzikarabati barabara zote, kuwajengea wananchi zahanati katika kata zote ili kupambana na magonjwa yanayoweza kuebukwa, kujenga shule na maabara ambayo yatawapa watoto wetu vifaa na ujuzi kwa kukabiliana na dunia hii ya teknolojia mpya, na kadharika.

Ukweli mwanana uliomo ni kwamba ushujaa siku hizi umebadirika na kubadirishwa. Badala ya kuwatumikia umma, viongozi na MPIgs wamegeuka na kuwa kasuku ili kuwasifia watawala wengine. Kila kiongozi anatafuta njia ya kupora mali ya umma. Umaahiri wa MPIGs kwa kunyemelea kasha la umma usiku wa manane wakati maskini wa Kambi Ya Mawingu(OlkalaU) walioadhiriwa na vurugu la 2007, wakaazi wa Korogocho, Kibera na Mukuru wamelala siyo ushujaa kamwe. Ni wizi bayana, ni uzingaombwe. Licha ya raslimali lukuki tulionayo, Kenya yaendelea kuzaa ushujaa wa viongozi walio na tamaa, walafi na kujipenda. Tunaongeza pato la taifa kila mwaka lakini lagawio viongozi badala ya kutumiwa kuleta maendeleo zaidi. Kama ningeulizwa, tungesherehekea siku ya leo kwa kuwakumbuka MPIGs wale 86 akiwemo pia BI. Baraza kwa kupiga hatua kubwa ya kuwakasilisha Wakenya mwezi ulipita.

Kukumbuka mashujaa kama MPIGs wale 86 ni sawa na kipofu anayemsaka paka mweusi kwenye chumba chenye giza ilhali paka huyo hayumo chumbani humo. Hawa ndio mashujaa wa leo, na wazalendo wanaohitaji kifagio ijapo mwaka wa 2013.

J. MTULIVU, mwanafunzi na mtukuzaji wa lugha yetu ya Kiswahili. Kiswahili kitukuke.

The views expressed on this op-ed/blog are solely those of the author and do not reflect the opinions of Mwakilishi News Media, or any other individual, organization, or institution. The content on this op-ed/blog is not intended to malign any religion, ethnic group, club, organization, company, or individual. The author himself is responsible for the content of the posts on this op-ed/blog, not any other organization or institution which he might be seen to represent. The author is not responsible, nor will he be held liable, for any statements made by others on this op-ed/blog in the op-ed blog comments, nor the laws which they may break in this country or their own, through their comments’ content, implication, and intent. The author reserves the right to delete comments if and when necessary. The author is not responsible for the content or activities of any sites linked from this op-ed/blog. Unless otherwise indicated, all translations and other content on here are original works of the op-ed/blog author and the copyrights for those works belong to the author.

Original Author: 
J. Mtulivu
Image: 

Post new comment

The content of this field is kept private and will not be shown publicly.
CAPTCHA
This question is for testing whether you are a human visitor and to prevent automated spam submissions to Mwakilishi.com.
Image CAPTCHA
Enter the characters shown in the image.

Follow us on Twitter @mwakilishi.

Featured Article

By Regina Njogu, Esq. - The bill's name is IRWAFA, which stands for Immigration Reform that Works for America’s Future Act. The bill has credibility because it is a bipartisan initiative and has the support of the White House as...

4395 reads

Featured Article

By Mary Kinuthia - For the young people out there, God gave us an opportunity to live in this country, Let us possess it and exploit our potential!!!

Many people know me as Karey. (Karey Kinuthia)  I’m only sharing my story to enco...

1816 reads

Featured Article

Beginning Wednesday May 1, entrants from the 2012 diversity visa (green card) lottery can check on-line at the U.S. State Department’s “Electronic Diversity Visa” Entrant Status Check (ESC) web site to see if they won.

Applicants need t...

4135 reads

Featured Article

If you have studied or are currently pursuing studies in Western countries, you have probably experienced some dim view about Africa, thanks largely to western media.

A Kenyan student studying at the Washington and Lee University in the...

1587 reads

SYNDICATED NEWS FEEDS

Aggregated Feeds