UhuRuto: Ushindi Keshaupata, Litafakarini Hili

Printer-friendly versionPDF version

Baada ya Wakenya kuwachagua viongozi wawapendao hapo wiki iliopita, akiwemo Rais Mteule Mhe Uhuru Kenyatta, bila shaka wananchi wanayatarajia mengi kutoka  kwao wakati huu. Aidha, sote tulishuhudia baadhi ya viongozi wakitimuliwa mbio na wengine wapya wakipewa madaraka na wapiga kura. Vigogo walioning'inia usukani kwa miongo mingi serikalini hadi wakadhania ya wao ndio waliokuwa bora, sasa hawamo nasi. Wote sasa wanatafuta kazi na kudodokwa na mate, huku wakimwandama Rais Mteule kokote aendapo, wakijifanya kuwa  wanamageuzi, wapenda mabadiliko, hadithi za kale hizo: nyani wale wale, misitu ile ile! Huh! 

Ushindi uliopatikana uliwasisimua Wakenya, na kusema kweli, tangu siku hio ya Jumatatu uchanguzi ulipofanyaka, Wakenya wengi walilala usingizi wa kaka Sungura, masaa mawili hapa, mengine matatu pale. Walifanya hivyo ili kufuatilia matokeo ya uchaguzi katika runinga,mtandaoni, magazetini, redioni na wengine kwenye porojo porojo za mashinani. Lakini sisi wananchi wa kawaida tunatarajia yapi kutoka kwa serikali ya UhuRuto? Pengine tutawasihi wayatende haya!

  1. Kuwaunganisha Wakenya wote ambao kidesturi na wakati wa uchaguzi, hupiga kambi katika hema zao za kikabila... na hukumbushwa jamii wanazotoka na viongozi wao. 
  2. Kati ya mawaziri ishirini na mmoja watakao chaguliwa katika wizara mbalimbali, mmoja wao awe kutoka kwa Wakenya walio walemavu. Kuna Wakenya walio na upungufu wa kuona, kusikia, kutembea, waliopooza, na kadharika, walio elimu ya hali ya juu na wanaofunza katika vyuo vikuu vya taifa vikiwemo vyuo vya walimu.
  3. Kati ya mawaziri waliosalia ishirini, mmoja au wawili hivi watoke kutoka jamii zilizosahaulika kama vile Warendille, Wadasanach, Wamursi, Wanyagatum, Wagabbra, Wahamar koke, na wengineo. Hata wao wapewe nafasi na kuhusishwa serikalini kama Katiba inavyoagiza. Sehemu wanazoishi zahitajika kuimarishwa na maisha yao kuboresha ili angalao wawafikie Wakenya wenzao kimaendeleo.
  4. Sehemu ambazo mshikamano wa vyama Jubilee ulikataliwa, kama vile mikoa ya Pwani, Nyanza ya Kusini, Kaskazini Mashariki, na kwingineko, pia kuwakilishwe serikalini.
  5. Kutowaingiza serikalini viongozi ambao walizihudumia serikali za Mzee Kenyatta, Baba Moi, na Emillio Kibaki ili kutibu ugonjwa wenye vya "Wale wale, wao wao." Badala yake, kuwachagua, kuwachunguza na kuwakagua mawaziri wapya na walio wageni ili nao wapewe nafasi ya kutumia vipawa na elimu yao.
  6. Kutowaingiza serikali viongozi ambao walikataliwa katakata na wapiga kura, hasa wabunge ambao walikuwa na madoea ya kujiongezea posho wakati sote tumelala usingizi wa pono.
  7. Kutokomeza ulaji rushwa hasa katika afisi za serikali kama vile za Forodha, Nyayo House, Ardhi house, Bandari ya Mombasa, barabarani  hasa pale wananchi wanapokwenda kutafuta huduma kutoka kwa watumishi wa serikali. Madudu haya yahitajika kutatuliwa mara moja na serikali ya UhuRuto.
  8. Kuzipa nguvu na uhuru  taasisi zote zilizoteuliwa na Katiba Mpya kama vile Tume Ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa(NCIC), Tume ya Haki, Ukweli Na Maridhiano(TIRC), Afisi ya Hakimu Mkuu Bw Willy Mutunga, Mkuu wa Idara ya Vikosi Vya Polisi, na zinginezo.
  9. Kutowachagua Wakenya wasio na maadili, waliotajwa katika kashfa au waliojihusisha na vitendo ambavyo vyaweza kuipa serikali yetu sifa mbaya.
  10. Wakati mataifa ya magharibi yanatishia kuiwekea serikali ya Kenya vikwazo vya hapa na pale, UhuRuto wanahitajika kujenga urafiki mpya na mataifa mengine yasio na mwelekeo na nia kama hizo, kwani wasipokielewa ni kwamba wao wanaihitaji Kenya kuliko vile Kenya  inapowahitaji wao.
  11. Kuzifungua sehemu zile ambazo hali ya uchukuzi umekuwa shida tangu uhuru kwa kuzikarabati barabara hizo. Nyingi ya sehemu hizo zina utajiri mwingi hasa wa ukuzaji wa vyakula. UhuRuto wakifanya hivyo, tabia ya vijana kukimbilia mijini kutafuta ajira itafika mwisho.
  12. Kuwatafutia Wakisii wanaochonga sanamu  wakitumia mali ghafi; kuanzisha kiwanda chenye  mashini za barafu kwa jamii ya Wajaluo ambao tangu uhuru, wanasafirisha samaki zao hadi mji wa Thika; kuboresha maisha ya jamii za Mijikenda wakiwemo pia wakazi wa mitaa ya Kibera, Lang'ata, Mathare ambao wamesahauliwa na serikalini moja hadi nyingine, na mwisho kusuluhisha matatizo ya jadi ya jamii ya Wakamba la tatizo la maji kwa kuwajengea mabwawa na kuwachimbia visima.
  13. Kutatua tatizo la mashamba hasa katika sehemu za Taita Taveta, huku Bw Ruto akimrudishia Bw Muteshi shamba analotuhumiwa alilinyakua. Kuwapa makazi ya kudumu kwa wale waliadhiriwa na vurugu ya 2007/2008. Uhuruto wakifanya hivyo, wapiga kura watang'oa mizizi ya ukabila na chuki kutoka mawazo yao ujapo uchaguzi ujao.
  14. Kupunguza safari ya kiholela holela za watumishi na  maafisa wa serikali, hasa mawaziri na badala yake kuweka kipaumbele elimu ya watoto wetu, hasa wale wa kutoka jamii zilizosahaulika.

Serikali ya UhuRuto ikifanya hivyo na mengine mengi, Wakenya watajawa na matumaini ya kujikwamua kutoka umaskini uliokidhiri, umaskini wa kutupwa na wakuchekwa. Azeni kuchapa  kazi, wananchi wanawatazama kama mapera yalioiva lakini yalioko juu juu na pembeni mwa mti. 

 By J. Mtulivu.

The views expressed on this op-ed/blog are solely those of the author and do not reflect the opinions of Mwakilishi News Media, or any other individual, organization, or institution. The content on this op-ed/blog is not intended to malign any religion, ethnic group, club, organization, company, or individual. The author himself is responsible for the content of the posts on this op-ed/blog, not any other organization or institution which he might be seen to represent. The author is not responsible, nor will he be held liable, for any statements made by others on this op-ed/blog in the op-ed blog comments, nor the laws which they may break in this country or their own, through their comments’ content, implication, and intent. The author reserves the right to delete comments if and when necessary. The author is not responsible for the content or activities of any sites linked from this op-ed/blog. Unless otherwise indicated, all translations and other content on here are original works of the op-ed/blog author and the copyrights for those works belong to the author.

Original Author: 
J. Mtulivu
Image: 

Post new comment

The content of this field is kept private and will not be shown publicly.
CAPTCHA
This question is for testing whether you are a human visitor and to prevent automated spam submissions to Mwakilishi.com.
Image CAPTCHA
Enter the characters shown in the image.

Follow us on Twitter @mwakilishi.

Featured Article

By Regina Njogu, Esq. - The bill's name is IRWAFA, which stands for Immigration Reform that Works for America’s Future Act. The bill has credibility because it is a bipartisan initiative and has the support of the White House as...

4414 reads

Featured Article

By Mary Kinuthia - For the young people out there, God gave us an opportunity to live in this country, Let us possess it and exploit our potential!!!

Many people know me as Karey. (Karey Kinuthia)  I’m only sharing my story to enco...

1839 reads

Featured Article

Beginning Wednesday May 1, entrants from the 2012 diversity visa (green card) lottery can check on-line at the U.S. State Department’s “Electronic Diversity Visa” Entrant Status Check (ESC) web site to see if they won.

Applicants need t...

4181 reads

Featured Article

If you have studied or are currently pursuing studies in Western countries, you have probably experienced some dim view about Africa, thanks largely to western media.

A Kenyan student studying at the Washington and Lee University in the...

1599 reads

SYNDICATED NEWS FEEDS

Aggregated Feeds