Primary links
- HOME
- NEWS
- OP-EDS/BLOGS
- HOT TOPICS
- ANNOUNCEMENTS
- LIVE TV
- MUSIC
- MUSIC VIDEOS
- NEWS VIDEOS
- DIASPORA VIDEOS
Wakati Papa Benedicto wa XVI alipotangaza nia yake ya kujiuzulu kutoka uongozi wa Kanisa la Katoliki, ulimwengu wote,, hasa waumini wake zaidi ya billioni moja, waliachwa wameduwazwa. Akiwa Papa wa kwanza kufanya hivyo katika kipindi cha miaka 700, sote tulibaki tukijiuliza ni yapi yaliomfanya kuchukua hatua hiyo ya dharura? Sababu alizozitoa kwa waumini kwamba hali yake ya kiakiri na kiafya haimruhusu tena kutoa wajibu wake wa kiroho kwa wafuasi wa kanisa halikuwatosheleza wengi. Ni bayana kwamba kilichomwelekeza kuafikia uamuzi huo kilitokana na kashfa ya kufunika maovu hasa yale yaliohusu mapadre kuwadhalilisha na kuwabaka watoto waliokuwa wakiwahudumia.
Hapo mwanzo mwanzo katika uongozi wa Kanisa lake la Kikatoliki, Papa Mstaafu Benedicto wa Kumi na Sita, aliyejulikana kuwa mpole wa ajabu, alisisitiza mara kwa mara kuwa katu hakupenda kuliongoza kanisa hilo. Papa huyu alijulikana kuwa na msimamo mkali hasa katika masuala ya kijamii na thiolojia yaliohusu ushoga na matumizi ya mipira katika utendaji wa ngono. Pia alijua kuwa yeye hangehimili vishindo vya viongozi wa Vatican kwani hisia zake zilimtakaza yeye kuwa mtumwa wa imani na kiroho.
Kujiuzuru kwake bila shaka kulitokana kwa yeye kutoelewana na watawala wa Vatican ambao hawakuegemea upande wake kwa masuala mbalimbali kama vile mageuzi katika uongozi wa kanisa la Katoliki, usuluhishaji wa kashfa za kifedha katika Makao Makuu ya kanisa hilo huko Vatican, kudorora kwa uchumi wa taifa la Italia ambao lilitegemea sana jiji la Vatican, uteuaji wa Papa kutoka nchi za nje ya Uropa hasa Italiano, ubakaji wa watoto na padre kote ulimwenguni, jinsi ya kukabiliana na mashtaka yaliowakilishwa na walioadhiriwa na wachungaji na jinsi ya kuibadilisha Kanisa la Katoliki ili liende sambamba na karne husika.
Huku tukimshangilia kiongozi mpya wa kanisa la Katoliki kwa hoihoi, nderemo na vifijo, waumini wanachangamshwa na unyenyekevu wa Papa Francis Wa Assissi, ambaye mara moja alichagua kumuenzi Mtakatifu Francis 1, ambaye aliacha mali na maisha ya kifahari kutoka kwa wazazi wake na kuishi maisha ya umaskini, huku akiwasaidia watu hohehahe waliokuwa na shida na wakiwemo wagonjwa. Kipenzi huyu wa maskini, ambaye aliishi maisha duni huku akiwa Kardinali wa jiji la Buenos Aires, alitumia basi na wananchi wa kawaida, licha ya kuwa wadhifa wake ulimruhusu yeye kubebwa na gari ghali na ya kifahari. Alitembea miguu ili kukutana na wanyonge katika mitaa ya maskini katika jiji hilo kubwa la Argentina, huku akijadiliana nao kuhusu majanga yaliowakabiri, siku nenda siku kuja.
Imani na uongozi wake katika Shirika la Kijesuit, ambalo hupeleka injili ya Yesu Kristo katika mitaa ya majengo poromoka ambayo yamo katika vitongoji vya miji kadhaa katika taifa lake la Argentina, bila shaka yatawafanya wengi kukimbilia kanisa la Katoliki ili kulishwa na Neno la Mungu. Kiongozi wa Shirika La Majesuit, Padri Federico Lombardi aliduwazwa na vile Makardinali 115 walivyoamua kumchagua Papa Jorge Mario Bergolio huku wakifahamu kwamba yeye alikuwa Mjesuit ambaye nyendo na sera zao hazikuwapendeza Wataliano na watawala wa Vatican. Ni bayana kwamba, Papa Francis Wa Kwanza atalitikisa jiji na watawala wa Vatican, nchi ya Italia na ulimwenguni kwa sera zake za kuwatetea maskini na msimamo wake wa kupinga ushoga na utumizi wa mipira katika kuzuia uzazi, utoaji mimba, pale atakapoanza kuchapa kazi hivi karibuni.
Litakalo leta changamoto ni pale atakapoamua kuitembelea taifa la Kenya hapo siku za badaye na kumhimiza Balozi wa Vatican nchini mwetu amruhusu kuwatembelea wakazi wa Mtaa wa Kibera unaojumuisha sehemu kama vile Gatwekera, Kambi Muru, Kangemi, Kianda, Kichiinjio, Kisumu Ndogo, Laini Saba, Lindi, Makina, Makongeni, Mashimoni, Mugumoini, Raila, Sarang'ombe, Silanga, Siranga, na mwishowe, Soweto Mashariki na Magharibi. Litakalo msononesha Papa Francis Wa Assissi ni pale alikapoyaona makaratasi yenye vinyezi yakipeperushwa angani na kutoa popote, miaka hamsini baada ya Kenya kupata Uhuru. Kunauwezekano viongozi wa maeneo hayo watajaribu kuwachimbia wakazi hawa, ambao hukumbukwa ifikapo uchaguzi, vyoo ili kuepusha aibu itakayo wakereketa kwa kutowapa wananchi wao mahitaji ya kawaida kama vile makazi bora, uchukuzi bora, maji safi na salama, vyoo, maeneo ya kuzoa takataka, shule bora vituo vya afya vya kuwashughulikia wanawake na watoto na mengineo. Hongera Papa Francis wa Kwanza, kwetu tunakuhitaji wewe kuliko jiji lililokuwa lako la Buenos Aires. Karibu!
By J. Mtulivu.
The views expressed on this op-ed/blog are solely those of the author and do not reflect the opinions of Mwakilishi News Media, or any other individual, organization, or institution. The content on this op-ed/blog is not intended to malign any religion, ethnic group, club, organization, company, or individual. The author himself is responsible for the content of the posts on this op-ed/blog, not any other organization or institution which he might be seen to represent. The author is not responsible, nor will he be held liable, for any statements made by others on this op-ed/blog in the op-ed blog comments, nor the laws which they may break in this country or their own, through their comments’ content, implication, and intent. The author reserves the right to delete comments if and when necessary. The author is not responsible for the content or activities of any sites linked from this op-ed/blog. Unless otherwise indicated, all translations and other content on here are original works of the op-ed/blog author and the copyrights for those works belong to the author.
Follow us on Twitter @mwakilishi.
By Regina Njogu, Esq. - The bill's name is IRWAFA, which stands for Immigration Reform that Works for America’s Future Act. The bill has credibility because it is a bipartisan initiative and has the support of the White House as...
By Mary Kinuthia - For the young people out there, God gave us an opportunity to live in this country, Let us possess it and exploit our potential!!!
Many people know me as Karey. (Karey Kinuthia) I’m only sharing my story to enco...
Beginning Wednesday May 1, entrants from the 2012 diversity visa (green card) lottery can check on-line at the U.S. State Department’s “Electronic Diversity Visa” Entrant Status Check (ESC) web site to see if they won.
Applicants need t...
If you have studied or are currently pursuing studies in Western countries, you have probably experienced some dim view about Africa, thanks largely to western media.
A Kenyan student studying at the Washington and Lee University in the...
Aggregated Feeds
Post new comment