- Add new comment
- 33 views
Wanabii wa maneno waneno wananena, "Iwepo ni Mashariki au Magharibi, nyumbani ndiko kwema." Hata hivyo kuna wengi ya Wakenya waishio ughaibuni ambayo huyu uneni kwao, ni mzaha tu. Lakini ukweli upo wapi? Bila hata kusita, ni ukweli kwamba, kwa njia moja au nyingine, sote tumekwama ijapo ni kuamua kuishi kuketi Marekani na kwinginepo, au kwendelea na maisha ya pata potea, yaani unafanya kazi usiku kucha, kasha unachopokea kinayeyuka punde tu unapoupokea mshahara huo.
Maisha hapo Marekani, zikiwemo nchi zinginezo za Magharibi, ni sarakasi ya pata potea, pata lilipia, au mzunguko wa kupata na kulipwa jasho lako, kasha zote zinawaendea wanaokupa huduma za kila aina. Na ukweli ni kwamba, wanaofaidika katika sokomoko hilo ni watengenezaji bidhaa unazozitumia wewe na wengineo wanaokupa huduma zinginezo za kila aina, ingawa nyingi huzihitaji, ila zenyewe zanahitajika. na ni baada ya miaka nenda, miaka rudi, ndipo wewe unapoaanza kujiuliza maswali, " Je, ni kweli kwamba maisha yangu yanazunguka kwa kasi katika sehemu ile ile tu?" Kulipa umeme, simu, maji, mahitaji ya nyumbani na jamaa yako, na kadharika.
Lakini hata hivyo, maswali chungu nzima yanakusokota na kukukera moyoni, " Nifanye lipi?" "Nichukue hatua gani kutatua masaibu yanayonisibu?" Je, nimtegemee yupi aniokoe kutoka janga hili nililojitumbukiza mwenyewe/" Ninapotazama Wamarekani katika nchi hii, maswali mengi hunijia. Wale waliotenda tendo la kuvunja sheria, waliowatariki wachumba wao, waliovuta au kutumia madawa ya madawa, au waliotenda hili na lile lililohifadhiwa katika maktaba ya walinda usalama na sheria, kweli wakaazi wa nchi hii wamo taabani.
Lakini kwetu tulotoka kwingineko, hali sio kama ya Wamarekani wa nchi hii. Nikisema tuna suluhisho makhususi ya kukabiliana, au kukwepa majanga yanayowakabili wengi, nitakuwa mbaya wa kusema yasiyo ya kweli. Ukweli wa mambo ni kuwa, ni muhimu kwetu sisi sote, kujitahadhali na kujitayarisha pale mambo yatakapogonga mwamba. Wengi hawatakubaliana nami, lakini ukweli ni kwamba" unapopanda mbegu"za maisha kwa kununua au kupata cheti cha kile utakachokiita chako, "Matumaini ya maisha yangu," kwa kupanda mbegu itakayokusaidia katika siku za baadaye.
Sio mwiko utakapokulazimu wewe kwa hili na lile. Ninachosema hapa kwamba, jipangia maisha yako ya baada, katika mazingira yatakayo kufaidi wewe. Lakini unapobaini kwamba maisha hayatobadirika hadi pale utakapojibizana na, zama mwenyewe. Lakini suluhisho kamili ni kufikiria na kuzungumzia sawa sawa, na pengine kufikiria jinsi utakapofunga virago vyako na kurudi tulikotoka miaka kadha iliopita. Je, yako ni yapi? Yangu kwangu imo tayari, hasa wakati huu ninapoelekea kustaafu. Je uko tayari? Yangu tu ni kukupungia mkono wa kwaheli hasa nnapochukua hatua ya kubadirisha wakati na masaibu mengine
By J. Idavethi
Comments
Umenena kama ustadhi. Tulijitakia makuu na mwiba wakujidunga hauna pole. Kujimudu tu bila mwelekeo ni utani na kitanzi hasa siku za uzeeni. Ni kweli na haki kupiga maisha msasa kama hayabainiki, basi jaribu lingine wakati mda bado upo.
Mwandishi huyu nimemtolea kofia juu nimekuwa mara mingi sana nikisema watu wafikirie
about kuinvest nyumba juu kumeendelea na vitu kama maploti,nyumba,mashamba
zinaendelea kupanda nawakenya wenye wako kenya ndio wanazinunua.So watu wa diaspora
hata kama wewe hunjisifu ati mimi ni citizen so sirudi just keep in mind n Go forbid ur caught
driving while drunk,Or accidentally u hit the guys u work for,or u hit a fellow while driving when ur tired???
Or u loose yr job n u stay for a long time without getting one especially kama ni professional one???Am trying
to say things happen n we know they have happened juu we have a story of so was deported etc etc.So it's good
to invest here home for the rainny day but again life is what u make it.Mwandishi thank u for reminding all of us
Majanga, kama matone ya mvua ,yapo kote ulimwenguni na hatuwezi kuyakwepa.Hivyo basi kurudi makwetu si ngome dhidi ya majanga haya.