Kenya Secures Third Sh210 Billion Eurobond After Successful Roadshow in the US, UK

Kenya has issued a new Eurobond worth Sh210 billion ($2.1 billion), the country's third in a period of five years.
The loan has been secured following a successful roadshow in the United States and the United Kingdom by National Treasury officials.
The bond has been sold in two tranches of 7 and 12 years with an amortization rate of seven and eight percent respectively.
The issue had an over-subscription of 452 percent having attracted bonds priced at Sh950 billion ($9.5 billion).
“Throughout the roadshow, the investors appreciated and welcomed the strong and resilient economic growth that Kenya has welcomed and the expected growth in 2019,” says National Treasury Cabinet Secretary Henry Rotich.
The government will use the funds to finance a number of key development projects, bridge the deficit in the national budget and service maturing loans.
This is Kenya's third entry in the International Debt Capital Markets following the issuance of bonds priced at Sh200 billion ($2 billion) in June 2014 and another worth Sh200 billion in February 2018.
Comments
Pale serikali ionapo kwamba…
Permalink
Pale serikali ionapo kwamba haikusanyi kodi ya kutosha ili kutekeleza miradi na mahitaji yake, suluhisho linaloikabiri ni kukopa Deni! Deni! Deni! Katika taarifa iliyotolewa na KRA, kitengo cha serikali kilichopewa jukumu la kuokota kodi nchini, ni kati ya Wakenya millioni mbili unusu na millioni tatu waliolipa kodi mwaka 2018. Kati ya Wakenya takriban millioni arubaini na tano, karibu Wakenya millioni tatu tu ndio walioonyesha wamelipa kodi ipasavyo. Hebu tulitafakari swala hilo. Tuseme idadi ya watoto, vijana na wale wasiokuwa na kazi ni millioni saba. Je, Wakenya millioni therathini na tano wako wapi? Tarakimu hio inaonyesha kinaganaga kwamba Wakenya millioni therathini na tano waligoma kulipa kodi, au walikataa kulipa kodi, au walichelewa kufanya hivyo. Lakini idadi hii ni kubwa pale ikilinganishwa na miradi na mzigo mkubwa ambao serikali imeubeba kama vile, kulipa mishahara mikubwa kwa wafanya kazi wake, kuzikarabati barabara na kutekeza miundo mbinu mingineo. Lakini nani talipa kodi ambazo ndizo hizo zinaibiwa mchana mchana kila kukicha? Nani atatoa hela zake wakati fisi wanaozikondolea macho wangali ofisini? Wananchi wana sababu zikutosha kutolipa kodi. Wezi wa pesa za vijana wa NYS wako wapi? Waliopora pesa za shirika la nafaka wako wapi? Walioagiza bidhaa kutoka nchi ya Brazil zilizokuwa na vyuma vya sumu, kama vile mahindi na sukari wako wapi. Waporaji wa mali ya mashirika ya serikali kama vile Kenya Power, Kenya Pipeline, Geothermal Development Authority, KETRACO WAKO WAPI? Magavana na maofisa wengine wa Kaunti waliopatikana wamepora mali ya umma wako wapi? Wabunge manguruwe wanaojiongezea mishahara wakati wapendao wamepelekwa wapi? Wabunge manguruwe waliopokea hongo ya shilingi elfu kumi ili kutokomeza mswaada uliowalenga walioagiza bidhaa za sumu nchini walifanywa nini? Ni maswala kama haya yanayomghadhabisha akina yahe, akiwemo Wanjiku. Diposa kila Mkenya anajiuliza, mbona nilipe kodi ili wachache waweze kugurumisha magari makubwa makubwa ya kifahari, nyumba za Pharao, ila sisi hatuna hata baiskeli? Na wezi wale wale ambao waling'ang'a billioni 21 za mabwawa ya Kimwarer, ndio pia wanaopewa jukumu ya kukopa shilingi billioni 210, waziibe tena, watokomee tena tuachwe tukilipa. Badala Uhuru kuchukua hatua mwafaka kulinda mali ya umma, kuwafunga walioziiba pesa zetu, kuwafikiria wananchi na vitita chungu nzima vya umaskini, anawaambia Wakenya kuhusu mkono utani wa Raila, tamaa za Kalonzo Musyoka, miradi minne mikubwa, na upuuzi mwingineo. Asicho kifahamu ni
kuwa Raila na Kalonzo wanachumbia tumbo zao tu. Uhuru pia aelewe kwamba uongozi bora uliotukuka ni ule unaowatumikia wananchi wanyonge, makabwela, na halaiki kubwa ya akina yahe wanaokumbwa na visingiti vingi katika hekaheka zao za kutafuta riziki ya kila siku. Kashfa na milungura tunazozishuhudia kila siku kutoka kwa viongozi hawa ni ishara kuwa rais Uhuru kamwe ni muoga wa kupita kiasi, au anawatumia wezi hawa kumuibia pesa zake za kustaafu. Wananchi wanamtarajia awe na ushakii(courage) mkubwa anapopambana na vita dhidi ya mafisadi ili kuboresha maisha ya Wakenya wanaofariki kwa njaa, magonjwa na shida zinginezo.
Add new comment